UMUHIMU WA KULALA NDANI YA NETI

Vincent Oluoch

Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaambukizwa na mbu wa jenasi Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya protisti Plasmodium. Mara nyingi ugonjwa huo huitwa “homa” tu, ingawa homa ni dalili yake mojawapo tu, pia kuna magonjwa mengi yanayosababisha homa.

Malaria inatokea katika maeneo ya kitropiki na yanayokaribia tropiki ikiwa ni pamoja na sehemu za Amerika, Asia na Afrika. Mwaka 2015 duniani kulikuwa na maambukizi milioni 214 ya malaria, na watu 438,000 walikufa, wengi wao (90%) wakiwa barani Afrika, hasa watoto wachanga katika mataifa ya kusini kwa jangwa la Sahara.

wanawake wajawazito haswa wanahimizwa kujikinga kutokana na malaria kwa ku lala ndani ya neti iliyotibiwa kwa dawa. Hii inawazuia kuumwa na mbu wa jenasi Anopheles unaosababisha malaria.

inasemekana kuwa maelfu ya watoto wanaaga kila siku kutokana na ugonjwa huu wa malaria. Vimelea hivyo huzaa ndani ya seli nyekundu za damu, na kusababisha dalili kama vile anemia, maumivu kidogo ya kichwa, shida ya kupumua, takikadia, n.k., aidha kuna dalili nyingine za jumla kama vile homa, baridi, kichefuchefu, ugonjwa kama mafua, na katika hali mbaya zaidi kupoteza fahamu na hata kifo.

Majaribio yamefanywa kuibuka na chanjo ya malaria bila mafanikio makuu, pamoja na kuibua mbinu za udhibiti wa kiajabu zaidi, kama vile kubadili viini tete vya mbu ili kuwafanya sugu kwa vimelea pia umefikiriwa. Ingawa utafiti unaendelea, hakuna chanjo inayopatikana sasa inayotoa ulinzi wa hali ya juu dhidi ya malaria hivyo basi watu wote wanahimizwa kulala ndani ya neti ilioyotibiwa ili kuzuia ugonjwa huu kwa kuenea.

 http://wp.me/p8zdPN-4

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s